Mapumziko wakati wa shooting ya Bwana ni nuru yangu eneo la chamazi Dar es salaam.
Wawa ni baadhi wa waanzilishi wa kwaya ya vijana kijitonyama. Picha hii ilipigwa katika
usharika wa kijitonyama mwaka 1999. Eneo hili kwa sasa kuna jengo la
kitega uchumi cha usharika.
Monday, February 3, 2014
Enzi hizo
Ijue Kwaya ya Vijana Kijitonyama
KWAYA YA VIJANA KIJITONYAMA LUTHERAN
UTANGULIZI
Ni
kikundi kilichoundwa kwa madhumuni ya kueneza injili kwa njia ya
uimbaji. Msukumo wa kuunda kikundi ulitokana na msukumo uliokuwa ndani
ya waanzilishi baada ya kuona nguvu ya uimbaji katika kuvuta wengi na
kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.
MADHUMUNI
- Kutangaza Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji
- Kuwasaidia watu wakue katika maadili mema kwa njia ya Neno la Mungu, maombi na ushirika
- Kujenga mahusiano mazuri miongoni watu wote
- Kushiriki katika maendeleo ya kijamii
- Kuinua na kuendeleza muziki wa injili
- Kutoa huduma ya uimbaji vyuoni na mashuleni
- Kutoa huduma kwa wajane, yatima na wasiojiweza
MAFANIKIO
Kwaya ya Vijana ambayo ilianzishwa zaidi miaka 10 iliyopita imeshiriki na kutoa huduma ya uimbaji sehemu zifuatazo:-
- Makanisani
- Mikutano ya injili
- Kumbukumbu za Martin Luther Jr. katika Ubalozi wa Marekani
- Ufunguzi wa ofisi mpya za Ubalozi wa Marekani
- Kumbukumbu ya uhuru wa marekani
- Kumbukumbu ya kulipuliwa ofisi za Ubalozi wa Marekani
- Matamasha ya uimbaji katika mikoa mbalimbali ya Tanzania
- Kwenye misiba kuwafariji Wafiwa
- Kwenye maharusi na sherehe mbalimbali za kumtukuza Mungu
- Katika utumishi wetu watu wengi wamebadilisha maisha yao na kupokea wokovu wa Mungu baada ya kusikia nyimbo zetu, na baadhi yao wamekuja kutushudia.
- Kwenye makongamano ya vyuo na shule za sekondari
- Mbali kufanya huduma za kiroho Kwaya pia imesaidia maendeleo ya kijamii kama ifuatavyo:-
- Huduma za Yatima na Wajane
- Imewasaidia baadhi ya vijana ambao hawakuwa na msaada wa kupata elimu kwa kuwalipia ada na wengi wamepata ajira nzuri baada ya kumaliza masomo yao
- Kuwatafutia ajira vijana wasiokuwa na ajira ndani na nje ya kwaya
MATATIZO
- Uchakavu na upungufu wa vyombo vya muziki umerudisha nyuma maendeleo ya huduma yetu kwa kiasi kikubwa.
- Kuna changamoto ya ajira kwa vijana wanaojiunga na kwaya mara kwa mara
OMBI
Ili kuiwezesha huduma hii nzuri isirudi nyuma bali isonge mbele kwanza tunahitaji maombi yako na pia msaada wa hali na mali.
Ijue kwaya ya vijana kijitonyama
KWAYA YA VIJANA KIJITONYAMA
MFUMO WA UIMBAJI KATIKA KWAYA YETU
Kama yalivyoandaliwa na:
Mwalimu wa kwaya; Gadiel Ketto.
October 16, 2002
Yafuatayo
ni mapendekezo ya taratibu za uimbaji katika kwaya ya vijana. Msukumo wa
mapendekezo
haya ni kuweka mfumo mzuri na madhubuti usio badilikabadilika kulingana na
mabadiliko yoyote yayoweza kutokea katika kwaya. Mabadiliko yaweza kusababiswa
na kubadilika kwa waimbaji, waalimu, au viongozi. Pia misukumo toka nje ya
kwaya yaweza pia kuleta mabadiliko. Hivyo ili tuweze kuwa na mfumo imara wa
uimbaji, tunapendekeza yafuatayo:-
1. AINA YA UIMBAJI
Aina ya
uimbaji ni ile inayombariki Mungu na wanadamu. Lakini wanadamu huwa wana
vionjo
vingi na vinavyotofautiana. Hivyo ili tuweze kumgusa kila mtu yafaa sisi kama
waimbaji au
wasanii tuweze kuangalia kuwa hadhira inataka nini kwa ujumala bila kuangalia
na kuridhisha sehemu tu ya kundi la watu. Faida yake ni kuwa ujumbe wetu katika
nyimbo utaweza kuyagusa makundi yote katika jamii na kufanikisha malengo yetu.
Kwa hiyo basi tuwe na uimbaji wa aina mbalimbali kama
vile pambio, nyimbo za haraka haraka, nyimbo za taratibu na nyimbo za kawaida
zilizozoeleka katika muziki wa kanisani.
2. NYIMBO
Kama kwaya tunapaswa kujifunza na kuimba nyimbo
mbalimbali. Ni vyema nyimbo zetu
zikawa katika
makundi yafuatayo:-
a).Nyimbo
za zamani (classic music)
Hizi ni
nyimbo zilizoandikwa zamani ambazo zina "melody" nzuri na ujumbe
mzuri.
Hizi
zifundishwe na.kuimbwa katika kwaya yetu.
b).Nyimbo
za kutunga / kuandika wenyewe (contemporary music).
Nyimbo hizi
ni nzuri zaidi, zinachochea ubunifu na vipaji tulivyonavyo. Ni vizuri
tukaandika na kuimba nyimbo kulingana na jamii ya sasa na kwa faida ya vizazi
vijavyo. Tukumbuke kuwa hata nyimbo za zamani tunazoimba leo ziliandikwa na
watu kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Kama babu
zetu wasingeandika tusingekuwa na nyimbo nzuri za kuimba kama
tunavyofahamu. Kwa hiyo tujue kuwa kama
hatutaandka nyimbo leo, watoto wetu hawatakuwa na kitu cha kujivunia ambacho
tumewarithisha kwa ajili ya Bwana. Pia tukwepe kuimba nyimbo za watu wengine,
walioandika wenyewe na kuimbwa na watu wengine kwa kuzingatia sheria ya
haki-miliki tukijua kuwa hata tukiimba hatuwezi kuzirekodi.
3. MUZIKI / ALA
(ACCOMPANIMENT)
Ni vizuri
kumwimbia Mungu kwa kutumia vyombo mbalimbali ambavyo vinasaidia
kuusindikiza
ujumbe. Vyombo hivyo ni kama gitaa, keyboard,
tarumbeta, ngoma, nk.
Inafaa kuwa
na utaratibu mzuri wa kuvitumia bila kuleta fujo na kelele katika uimbaji. Hili
tu litawezekana endapo tutatafuta na kuwaandaa wanamuziki wetu katika kwaya hii.
4. UFUNDISHAJI WA NYIMBO
Kwaya nzuri ni ile yenye waalimu wengi angalau watano
wenye vipaji na utaalamu katika fani ya muziki. Hawa lazima wawe na sauti moja
ili kifanya kwaya iwe moja uimbaji mmoja na usiobadilika. Kiburi na kujikweza
iwe mwiko kwa walimu wa kwaya hii. Pia kuwe na utaratibu mzuri wa kufundisha
nyimbo kwa kupeana nafasi na kushirikiana katika kuboresha. Kwa upande huu pia
ni vyema wale wenye vipaji wakatiwa moyo ili kusomea fani ya muziki.
5. UBORESHAJI WA UIMBAJI
Kama waswahili wasemavyo ukiamua kumla nguruwe chagua
aliyenona, vivyohivyo na
sisi kama tumenamua kuimba ni vyema tukaimba vizuri. Hivyo ni
vizuri tukazingatia mazoezi ya mara kwa mara ya uimbaji na kuhakikisha kuwa
kila mwanakwaya anashiriki. Mazoezi haya yafanyike kila siku za mazoezi,
kuandaa kambi, na hata kufanya mikesha maaalumu ya mazoezi ya uimbaji.
Friday, January 31, 2014
Monday, March 19, 2012
Mungu ni mwema
Karibuni wote
Subscribe to:
Comments (Atom)

