Monday, February 3, 2014

Ijue Kwaya ya Vijana Kijitonyama

KWAYA YA VIJANA KIJITONYAMA LUTHERAN
UTANGULIZI
Ni kikundi kilichoundwa kwa madhumuni ya kueneza injili kwa njia ya uimbaji. Msukumo wa kuunda kikundi ulitokana na msukumo uliokuwa ndani ya waanzilishi baada ya kuona nguvu ya uimbaji katika kuvuta wengi na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.
MADHUMUNI
  • Kutangaza Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji
  • Kuwasaidia watu wakue katika maadili mema kwa njia ya Neno la Mungu, maombi na ushirika
  • Kujenga mahusiano mazuri miongoni watu wote
  • Kushiriki katika maendeleo ya kijamii
  • Kuinua na kuendeleza muziki wa injili
  • Kutoa huduma ya uimbaji vyuoni na mashuleni
  • Kutoa huduma kwa wajane, yatima na wasiojiweza
MAFANIKIO
Kwaya ya Vijana ambayo ilianzishwa zaidi miaka 10 iliyopita imeshiriki na kutoa huduma ya uimbaji sehemu zifuatazo:-
  • Makanisani
  • Mikutano ya injili
  • Kumbukumbu za Martin Luther Jr. katika Ubalozi wa Marekani
  • Ufunguzi wa ofisi mpya za Ubalozi wa Marekani
  • Kumbukumbu ya uhuru wa marekani
  • Kumbukumbu ya kulipuliwa ofisi za Ubalozi wa Marekani
  • Matamasha ya uimbaji katika mikoa mbalimbali ya Tanzania
  • Kwenye misiba kuwafariji Wafiwa
  • Kwenye maharusi na sherehe mbalimbali za kumtukuza Mungu
  • Katika utumishi wetu watu wengi wamebadilisha maisha yao na kupokea wokovu wa Mungu baada ya kusikia nyimbo zetu, na baadhi yao wamekuja kutushudia.
  • Kwenye makongamano ya vyuo na shule za sekondari
  • Mbali kufanya huduma za kiroho Kwaya pia imesaidia maendeleo ya kijamii kama ifuatavyo:-
  1.     Huduma za Yatima na Wajane
  2.    Imewasaidia baadhi ya vijana ambao hawakuwa na msaada wa kupata elimu kwa kuwalipia ada na wengi wamepata ajira nzuri baada ya kumaliza masomo yao
  3.     Kuwatafutia ajira vijana wasiokuwa na ajira ndani na nje ya kwaya
MATATIZO
  • Uchakavu na upungufu wa vyombo vya muziki umerudisha nyuma maendeleo ya huduma yetu kwa kiasi kikubwa.
  • Kuna changamoto ya ajira kwa vijana wanaojiunga na kwaya mara kwa mara
OMBI
Ili kuiwezesha huduma hii nzuri isirudi nyuma bali isonge mbele kwanza tunahitaji maombi yako na pia msaada wa hali na mali.

No comments:

Post a Comment