KWAYA
YA VIJANA KIJITONYAMA LUTHERAN
UTANGULIZI
Ni
kikundi kilichoundwa kwa madhumuni ya kueneza injili kwa njia ya uimbaji.
Msukumo wa kuunda kikundi ulitokana na msukumo uliokuwa ndani ya waanzilishi
baada ya kuona nguvu ya uimbaji katika kuvuta wengi na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.
MADHUMUNI
- Kutangaza Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji
- Kuwasaidia watu wakue katika maadili mema kwa njia ya Neno la Mungu, maombi na ushirika
- Kujenga mahusiano mazuri miongoni watu wote
- Kushiriki katika maendeleo ya kijamii
- Kuinua na kuendeleza muziki wa injili
- Kutoa huduma ya uimbaji vyuoni na mashuleni
- Kutoa huduma kwa wajane, yatima na wasiojiweza
MAFANIKIO
Kwaya
ya Vijana ambayo ilianzishwa miaka 10 iliyopita hushiriki kutoa huduma ya
uimbaji sehemu zifuatazo:-
- Makanisani
- Mikutano ya injili
- Kumbukumbu za Martin Luther Jr. katika Ubalozi wa Marekani
- Ufunguzi wa ofisi mpya za Ubalozi wa Marekani
- Kumbukumbu ya kulipuliwa ofisi za Ubalozi wa Marekani
- Matamasha ya uimbaji katika mikoa mbalimbali ya Tanzania
- Kwenye misiba kuwafariji Wafiwa
- Kwenye maharusi na sherehe mbalimbali za kumtukuza Mungu
- Katika utumishi wetu watu wengi wamebadilisha maisha yao na kupokea wokovu wa Mungu baada ya kusikia nyimbo zetu, na baadhi yao wamekuja kutushudia.
- Kwenye makongamano ya vyuo na shule za sekondari
- Mbali kufanya huduma za kiroho Kwaya pia imesaidia maendeleo ya kijamii kama ifuatavyo:-
Ø Huduma za Yatima
na Wajane
Ø Imewasaidia
baadhi ya vijana ambao hawakuwa na msaada wa kupata elimu kwa kuwalipia ada na
wengi wamepata ajira nzuri baada ya kumaliza masomo yao
Ø Kuwatafutia ajira vijana wasiokuwa na ajira ndani na
nje ya kwaya
MATATIZO
Uchakavu
na upungufu wa vyombo vya muziki umerudisha nyuma maendeleo ya huduma yetu kwa
kiasi kikubwa. Kwaya inashindwa kutoa huduma vizuri ibabadi au inapopata
mialiko. Kwa mfano maranyingi vyombo hugoma wakati tupo jukwaani, jambo ambali
huleta fedheha sio tu kwa wanakwaya bali hata wale waliotualika au wanaosubiri
huduma yetu. Kwa sasa kwaya imesitisha kupokea mialiko na kufanya huduma sehemu
mbalimbali kutokana na ubovu wa vyombo labda pale tunapofanikiwa kuazima au
kukodi vyombo vya muziki.
OMBI
Ili
kuiwezesha huduma hii nzuri isirudi nyuma bali isonge mbele tunaomba msaada
wako wa kutuchangia vyombo kulingana na listi iliyoambatishwa.
No comments:
Post a Comment